Wednesday , 9th Nov , 2022

Agizo la waziri mkuu la kufufua visima vilivyopo jiji Dar-Es-Salaam Bado linaendelea kutekelezwaa na Wakala wauchimbaji visima na ujenzi wa mabwawa-DDCA Kwa kushirikiana na mamlaka ya maji na Usafi wa mazingira-DAWASA  ambapo  Hadi sasa tayari visima zaidi ya 50 vimesafishwa.

Huu ni mwendelezo na timu imefika  Tabata Jijini Dar es Salaam harakati zinaendelea kuvisaka na kuvirudisha katika ramani visima Ili kuepuka adha ya maji iliyopo Kwa sasa  jijini Dar-Es-Salaam katika ufufuzi huo Afisa mwenezi kutoka DDCA  Renatus Manoga amesecma kwamba zoezi hilo limeanza rasmi ijumaa ya wiki  iliyopita na tayari  vimeshaunganishwa kwenye mtandao wa DAWASA.

Wataalamu hao kutoka serikalini wamesema mashine wanazotumia kufufua visima hivyo zinauwezo wa kuchimba Hadi mita mia nne hamsini kwenda chini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa kisiwani kata ya Tabata Alhaj Rajib mbwana Chala ameeleza kwamba  kisima hicho kilikuwepo tangu miaka kumi na tano iliyopita na kilikuwa hakitumiki baada ya kupatikana Kwa maji ya dawasa hivyo kufufuliwa kwake kutatua changamoto ya uhaba wa Maji Kwa wakazi wa eneo hilo.