
Basi la abiria lililopata ajali
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kwamba kati ya sita waliofariki dunia, wanne wametambulika na waliojeruhiwa wanawake ni 10 na wanaume 12.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa wa Dodoma, Dkt Ernest, amesema kwamba majeruhi 17 waliopokelewa katika hospitali hiyo wanaendelea vizuri.