Sunday , 13th Nov , 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, ameeleza kuwa uongozi bora wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amani iliyopo nchini Tanzania ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji kwenye sekta ya utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Iringa.

Amesema  Tanzania imejaliwa kuwa na vizutio vingi, Bara na Visiwani, hivyo wawekezaji wa ndani na nje wachangamkie fursa hiyo kwani baada ya Janga la UVIKO 19 nchi imefunguka na watalii wanaingia kwa wingi nchini ambapo wanahitaji huduma mbalimbali.

Aidha, katika kongamano hilo lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Othman Masoud,  Mhe. Balozi Dkt. Chana, amewaahidi wawekezaji kuwa, Wizara anayoiongoza itaendelea kushirikiana nao, katika kuweka Mazingira mazuri na rafiki ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii nchini.