
Rais wa Marekani Joe Biden katika hotuba yake amezungumzia umuhimu wa kuepuka migogoro kati ya Marekani na China huku akisema ni muhimu nchi hizo zifanye kazi pamoja katika masuala ya dharura ya kimataifa ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa usalama
Mkutano huu unafanyika pembezoni mwa mkutano wa nchi ishirini zilizoendelea na zinazoendelea kiviwanda G20 na ndio wa kwanza kwa viongozi hao wawili kukutana ana kwa ana tangu Biden alipochukua hatamu za uongozi Marekani.