Monday , 14th Nov , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, amesema licha ya uwepo wa sheria na kanuni za kuwadhibiti wachafuzi wa mazingira hususani wanaotupa taka hovyo ni vyema pia ikaenda sambamba na kuwazomea Kama sehemu ya kuwafanya wajisikie aibu kwa kosa walilofanya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

RC Makalla ametoa kauli hiyo leo Novemba 14, 2022, wakati wa kikao kazi na viongozi wa wilaya wakiwemo wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Meya na maafisa mazingira kilichoketi kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi kulingana master plan ya mkoa na mikakati endelevu ya kuimarisha suala la usafi na utunzaji wa mazingira.

Aidha RC Makalla ameelekeza watendaji kuanzia ngazi ya mtaa kuhakikisha wanabeba jukumu la usafi kwa kuweka mkazo kwenye kampeni ya usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi na kudhibiti machinga kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Halmashauri za mkoa huo kuangalia upya suala la utoaji wa mikataba ya muda mrefu kwa wakandarasi wa usafi ili waweze kukopesheka na kununua vifaa vya kisasa tofauti na sasa ambapo wanapatiwa mikataba ya muda mfupi.