Monday , 14th Nov , 2022

Vyama vya upinzani na asasi za kiraia nchini Mexico wamejitokeza m    mitaani kuandamana kupinga mabadiliko ya tume ya uchaguzi yanayokusudiwa kufanywa na Rais wa nchi hiyo Andres Manuel Lopez Obrador

Rais huyo alipendekeza mabadiliko ya masuala ya uchaguzi ambayo yatabadilisha tume ya uchaguzi ya nchi hiyo

Rais Andres anasisitiza kuwa taasisi hiyo inashikiliwa na watu wenye ushawishi, lakini wapinzani wanasema mabadiliko hayo yataondoa nguvu yake ya kuwa huru na kuifanya kuwa ya kisiasa zaidi.