Tuesday , 15th Nov , 2022

Watu sita wa familia ya Mchungaji wa Kanisa la Baptist Itezi  jijini Mbeya Daniel Mwandenga, wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijulikana.

Akizungumzia tukio hilo, Mke wa Mchungaji Rebeka Mwandenga amesema moto huo umezuka ghafla Novemba 14, majira ya saa 12 jioni  katika moja ya chumba ambacho hakikuwa na umeme  wala nishati nyingine na kusambaa kwenye nyumba yote na kutekeleza vitu vyote vilivyokuwa ndani.

Mwenyekiti wa Mtaa wa  Itezi Mashariki, Michael Kwimba amesema  amepata taarifa za tukio hilo kwa kuchelewa na kwamba alipofika eneo la tukio alikuta wananchi wakiendelea na jitihada za kuuzima moto huo