
Imeelezwa kuwa Adnan Oktar, aliongoza vipindi vya televisheni akionekana kuzungukwa na wanawake waliokuwa wamevaa nguo ambazo hazikuwa zikiwastiri vyema
Kiongozi huyo amekuwa akituhumiwa kujihusisha na masuala ya unyanyasaji wa kingono ambapo pia mwaka jana, alihukumiwa kifungo cha miaka 1,075 kwa sababu ya manyanyaso ya kingono kwa watoto wadogo na makosa mengine, hukumu ambayo baadae ilibatilishwa na mahakama
Oktar amejizolea umaarufu kwa vipindi vyake vilivyorushwa kupitia televisheni ya A9 kwa njia ya mtandao alivyokuwa akionekana na wanawake mbalimbali wengine wakicheza mbele yake huku wakifanya mazungumzo kitendo ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakiona ni kinyume na maadili