
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa ACP - Theopista Mallya anasema watuhumiwa 95 walikamatwa katika Wilaya ya Nkasi na watuhumiwa 78 katika Wilaya ya Kalambo
Inaelezwa kuwa watu hao wamekuwa wakichochea vitendi hivyo vya kishirikina na kusababisha uvunjifu wa amani katika mkoa huo ambapo tayari watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani
Katika hatua nyingine jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya Gobole kinyume na sheria, mwingine na Nyara za serikali ambazo ni Ngozi ya Paka Pori na mtuhumiwa mwingine amekamatwa akiwa na vitu ambavyo vinazaniwa kuwa vya wizi zikiwemo TV 3 na Redio Moja.