Monday , 21st Nov , 2022

#HABARI Waziri wa habari na mawasiliano Nape Nnauye  ameyataka makampuni yanayotoa Huduma za mawasiliano kutoongeza gharama za bando ama kufanya mabadiliko yeyote mpaka pale tathimini itakapokamilika

Nape ametoa kauli hiyo ya serikali ambapo amesema tathimini ya mwisho ilifanyika mwaka  2018 na nyingine inafanyika mwaka huu ikitegemewa kukamilika kati ya mwezi December na Januari

Nape amesema Kwa sasa Hali inaonesha kutokuwepo Kwa mahusiano mazuri kati ya watoa huduma na watumiaji wa Huduma za mawasiliano hivyo serikali imeamua kufanya tathimini ya kina ambayo itakuja na majibu ya gharama gani zitumike kwenye bando usafirishaji wa data,ulipaji wa Kodi uwekezaji na masuala mengi ya kiuendeshaji