
Miongoni mwa nyumba zinazotakiwa kubomolewa
Wananchi hao wameeleza kuwa waliambiwa kuwa wanapewa notisi ya kuondoka ndani ya siku 14.
Wakizungumza na EATV baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo wamesema Novemba 11 mwaka huu walipokea barua kutoka kwa Afisa mtendaji wa kijiji cha Kahunda Karoli Theodory kuwa wabomoe nyumba zao ili kupisha upanuzi wa barabara na ujenzi wa soko.
’’baada ya kuletewa barua ya kubomoa na kitongoji nilienda ofisini kulalamika kwanini niletewe barua ya kubomoa wakati niliuziwa na Kijiji eti barabara, wakati nanunua uongozi hawakujua kama kuna barabara? Kuna unyanyasaji unaojitokeza kuna viongozi wanatunyanyasa sisis watu wa hali ya chini na kama kuna Waziri wa tamisemi atusaidie na hatuwezi kupiga maendeleo lakini watushirikishe sikuambiwa kama kuna barabara hapa ’’ amesema Hussein Kapemba, Mkazi wa Kijiji cha Kahunda
Julius Mulongo ni kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Buchosa akatolea ufafanuzi malalamiko ya wakazi hao akibainisha kuwa serikali ya kijiji ndio imeratibu zoezi hilo baada ya kukaa kikao na wanakijiji, akisisitiza serikali ya kijiji ndio ilikuwa na maamuzi ya kufanya hivyo.