Monday , 21st Nov , 2022

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai LengaI Ole Sabaya, kwa mara nyingine umeshindwa kuwasilisha hati ya kisheria kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini DPP baada ya Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani

Hati hiyo inaruhusu Mahakama ya Hakimu Mkazi kusikiliza shauri la uhujumu uchumi na inapaswa kupokelewa na Hakimu Salome Mashasha ambaye anasikilia shauri hilo.