Monday , 21st Nov , 2022

Jeshi la Polisi nchini limesema Novemba 22, 2022, litateketeza silaha haramu zilizosalimishwa kwa hiari katika kampeni maalumu iliyofanyika nchi nzima kuanzia Septemba 01 hadi Oktoba 31 mwaka huu iliyokuwa ikiongozwa na kauli mbiu isemayo "Silaha haramu sasa basi, salimisha kwa hiari".

Silaha haramu zitakazoteketezwa

Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 20, 2022, na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime, ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kuanzia muda wa saa 2:00 asubuhi katika viwanja vya shabaha vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vilivyopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.

Aidha amebainisha kuwa Mgeni rasmi katika zoezi hilo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, na wananchi wote wanakaribishwa kujionea.