
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa Nasoro Athuman mwaka 2020, alimuua kwa silaha mwendesha bodaboda aitwaye Nurdin Athuman maeneo ya Mji mpya Manispaa ya Morogoro, kisha kuondoka na pikipiki pamoja na simu ya marehemu.
Mtuhumiwa mwingine Abdallah Ramadhan alimuua mwendesha pikipiki Emmanuel Leons mwaka 2020 katika maeneo ya Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
Kwa mjibu wa Jaji Gembe, Nassoro Athumani amekaa mahabusu kwa miaka miwilli na miezi nane, atatumikia adhabu ya kifungo chake katika gereza la wami, ili kumwezesha kujifunza ujuzi mbalimbali utakao msaidia baada ya kifungo chake kujitafutia kipato.
Imeelezwa kuwa, Abdallah Ramadhan kabla ya kutekeleza mauaji hayo, alimkodi mwendesha pikipiki huyo kwa madai ya kumpeleka mahala ambapo baada ya mwendo kupita alitumia nafasi hiyo kufanya mauaji na kuondoka na pikipiki, ambapo baadae alitiwa mbaroni na vyombo vya dola.
Washitakiwa wote wamekiri kufanya mauaji hayo, mahakama ikitoa hukumu kisheria kupitia kifungu namba 198 cha kanuni ya adhabu, ambapo katika kesi namba 59 ya mwaka 2022 imeendeshwa na wakili wa serikali Emmanuel Kaigi huku upande utetezi ukiwa na wakili Ignas Punge, kesi No. 95/2022 ikiendeshwa na Wakili wa serikali Emmanuel Kaigi huku upande utetezi ukiwa na wakili Daud Malya.