
Mtu anayeaminika kuwa meneja wa duka alifyatua risasi kisha akajigeuzia bunduki, na kujiua.
Polisi katika Jiji la Chesapeake wamethibirtisha kutokea kwa mauaji hayo kupitia ujumbe wa Twitter.Kuna maelezo machache, lakini afisa mmoja wa polisi alizungumzia kuhusu watu wasiozidi 10 waliouawa na wengine wengi kujeruhiwa. Sababu ya mauaji hayo haijawekwa wazi…
Picha za video zilionekana mtandaoni ambazo zilionekana kumuonesha shuhuda - akiwa amevalia sare za Walmart akielezea kilichotokea.
Alisema aliondoka katika chumba cha wafanyakazi, ambacho meneja aliingia na kufyatua risasi.
Polisi walitarajiwa kutoa taarifa zaidi hii leo juu ya tukio hilo.