Tuesday , 6th Dec , 2022

Wafanyabiashara wa nyama kwenye mabucha yaliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, wanalazimika kuuza kilo moja ya nyama kwa 6000 kutoka 8000 kutokana na kukosekana kwa wateja huku wakieleza kwamba changamoto ya ukosefu wa majokofu ya kuhifadhia nyama kunachangia kuuza kwa bei ya hasara.

Nyama

Wakizungumza leo Desemba 06, 2022, na East Africa TV wafanyabiashara hao wamesema kuna haja ya soko la nyama kuongezewa thamani kwa kuuzwa kwenye nchi nyingi tofauti na sasa kwani Tanzania imekuwa na idadi kubwa ya Ng'ombe lakini soko limekuwa dogo 

Wamesema licha ya kuboreshewa bucha za kufanya biashara hiyo tofauti na awali lakini hali ya kibiashara kwao imekuwa ngumu

Kwa upande wake daktari wa nyama kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, anayesimamia eneo la bucha za nyama Vingunguti, Dkt David Gabriel, amesema hawaruhusu kuingizwa Kwa nyama ya Ng'ombe kuingizwa kwenye bucha hizo bila ya kuwa na muhuri maalum wa serikali unaoelekeza kama nyama husika imekaguliwa na ni salama kwa mlaji