Akitoa ombi la kuahirishwa kwa kesi hiyo wakili Erick Mutta anayewakilisha jopo la mawakili wanaomtetea Mfalme
Zumaridi na wafuasi wake hao amesema shahidi huyo kwa jina Anitha Wambola amebanwa ghafla na kifua hivyo kukosa uwezo wa kutoa ushahidi wake hali iliyopelekea kuomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine ili shahidi huyo apate muda wa kupata matibabu
Hakimu Monica Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Desemba 08/2022
Aidha shauri namba 11 la usafirishaji haramu wa binadamu linalomkabili mfalme Zumaridi peke yake limehairishwa hadi kesho kutokana na ushahidi wake kutokamilika