
Inaelezwa kuwa Balozi Mushy alifariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amethibitisha kifo cha Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy aliyepata ajali Wilayani humo huku akisema kuwa mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua
"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Balozi huyo
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Balozi Celestine Mushi, Balozi wa Tanzania nchini Austria na Mwakilishi wa Kudumu wa nchi yetu katika Mashirika ya Kimataifa, Vienna. Tumeondokewa na mwanadiplomasia mahiri na mtumishi makini wa umma. Mungu amweke mahali pema. Amina" ameandika Rais Samia