
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova
Urusi imesema kuwa kitendo cha Marekani kuisaidia Ukraine ni kama uchokozi na hawatasita kujibu
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova, amesema hatua ya Marekani kupeleka makombora ya kujilinda na kunasa makombora ya Urusi ni kama marekani inatangaza kuingia moja kwa moja katika mgogoro
Tayari Marekani imetoa mafunzo kwa karibu wanajeshi 3,100 wa Ukraine, namna ya kutumia silaha hizo
Wakati hayo yakijiri tayari Marekani imewekea Russia vikwazo vipya vya kiuchumi na safari hii vimemlenga mfanyabiashara tajiri nchini humo Vladimir Potanin na familia yake
Hatua hiyo inalenga kuishinkiza Moscow kuachana na vita vyake nchini Ukraine.
Potanin, aliwahi kuwa naibu wa waziri mkuu wa Russia, na Marekani imesema kwamba ana uhusiano wa moja kwa moja na rais wa Russia Vladimir Putin.
Wizara ya fedha ya Marekani pia imewekea vikwazo benki ya biashara ya Russia ya Rosbank ambayo Potanin alipata haki za umiliki wake mapema mwaka huu pamoja matawi 17 ya benki ya VTB ambayo ndio benki kubwa zaidi nchini Russia