Tuesday , 27th Dec , 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana, ameendelea kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana

Huku yeye mwenyewe akishiriki kwa vitendo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani.

Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa wananchi waendelee kulinda na kutunza vivutio vya maliasili ambavyo Tanzania imejaaliwa ili viendelee kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema  Hifadhi ya Taifa ya Saadani ina vivutio vingi na vya kipekee zikiwemo fukwe za Bahari ya Hindi pia inafikika kwa urahisi kutokana na  uwepo wa miundombinu rafiki kama vile reli iliyopita katika hifadhi inayowezesha watalii kufika vyema na kujionea vivutio mbalimbali.