Korosho zilizobanguliwa
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Koroshi nchini, Francis Alfred, ambapo pamoja na mambo mengine amesema, kupatikana kwa soko hilo kutaongeza thamani ya zao la korosho na kuongeza kipato kwa wakulima.
Awali mkuu wa wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala, akawataka wakulima kuongeza uzalishaji, na kwamba kupitia uwekezaji huo, serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji, huku meneja wa kiwanda akaeleza kupitia ubanguaji huo, namna ambavyo kiwanda hicho kimetoa ajira kwa wananchi.