Wednesday , 28th Dec , 2022

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imepanga Januari 17,2023 kuendelea kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi 

Akiahirisha rufaa hiyo  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa amesema  rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa Januari 17 na kabla ya siku hiyo itatajwa Januari 9, 2023 ili kuona kama tangazo limetolewa kwa wajibu rufaa wawili ambao hadi sasa hawajafika mahakamani

Katika rufaa hiyo namba 155/2022 inayosikilizwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha,m bali na Sabaya wajibu rufaa wengine ni Enock Mnkeni, John Aweyo, Sylvester Nyegu,Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mbali na Sabaya ambaye amewakilishwa na wakili Fauzia Mustafa ,mjibu rufaa wa pili (Mnkeni) alikuwepo mahakamani hapo,huku mjibu rufaa wa tatu (Aweyo) ambaye hakuwepo mahakamani hapo akiwakilishwa na wakili Fridolin Bwemelo.

Hakimu Mbelwa amseema kwa kuwa matangazo ya hati ya wito mahakamani yameshatolewa mara mbili,yatatolewa kwa mara ya tatu ili wajibu rufaa wawili ambao ni Macha na Msuya waweze kufika mahakamani na shauri hilo kuendelea kusikiliza kwa tarehe iliyopangwa.

Wakili Bwemelo kwa niaba ya mteja wake na Mnkeni ambaye hakuwa na uwakilishi mahakamani hapo  wameomba kupatiwa mwenendo,hukumu na nakala za vielelezo vilivyotolewa katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 na mahakama ya chini ili waweze kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa.

Nae Wakili Fauzia  anaemwakilisha  mjibu RUFAa wa kwanza Lengai ole Sabayaameomba   kupatiwa nakala ya vielelezo vilivyotolewa katika kesi hiyo ,iliyokuwa inasikilizwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,hati ya mashitaka ya kwanza pamoja na hati ya pili iliyofanyiwa marekebisho.

Wakili wa Serikali mwandamizi,Akisa Mhando,anayemwakilisha mjibu rufaa,aliiomba mahakama kutaja shauri hilo Januari 9,2023 kabla ya tarehe ya kusikilizwa ili kuona endapo tangazo limetolewa na wahusika wamelipata.

Rufaa hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake watano inapinga hukumu iliyotolewa Juni 10,2022  na Hakimu Mkazi Patricia Kisinda wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ,hukumu iliyowaachia Sabaya na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi  namba 27/2021 katika mahakama hiyo ya chini