Azam Fc
Akizungumza na EATV, Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe amesema bado wapo kwenye harakati za kuhakikisha wanaondoka na alama 3 kwenye michezo 8 iliyosalia huku akisifu uwezo wa kikosi chao
''Tuna kikosi imara naamini tutapata matokeo mazuri ambayo yatatuweka katika nafasi nzuri ''Hasheem Ibwe
Kwa upande mwingine ,Ibwe ameelezea maandalizi ya kikosi chao kuelekea michezo iliyosalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imesimama kidogo kupisha ushiriki wa klabu za Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa
Azam Fc inakamata nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 43 huku mchezo unaofuata kwenye mzunguko wa 24 watapambana na Simba SC mnamo Februari 21-2023 kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya Saa 19:00 Usiku



