Madume ya ng’ombe 36 aina ya Boran Heifer
ili kupata mbegu bora ya ng’ombe watakaozaliwa kupitia madume hayo na kuondokana na ufugaji wa ng’ombe wa asili wasio na tija.
Akiwa Misungwi Mwanza Ulega amesema Tanzania ina ng’ombe milioni 33 na bado tija ipo chini sana kutokana na viwanda vingi kutopata malighafi ya kutosha.
Ameongeza kuwa kupitia programu maalum ya Samia Ufugaji kwa Tija (SAUTI), serikali imefanikisha kuanzisha mafunzo ya unenepeshaji mifugo ambapo takriban vijana 70 wanapatiwa mafunzo hayo kwa vitendo katika Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Wilayani Misungwi.

Aidha amesema serikali imeanzisha vituo atamizi vya SAUTI ambapo mpaka sasa kuna vituo nane kwa ajili ya vijana kufunzwa.
Amesema pia kupitia vituo hivyo atamizi vijana watafundishwa namna bora na kisasa ya kutengeneza mashamba ya malisho na upatikanaji wa mifugo bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga aliishukuru serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipata ng’ombe kwa halmashauri ya Buchosa huku mmoja wa wanafunzi hao ameishukuru serikali kwa kuja na programu hiyo ya ufugaji ambayo itawasaidia kupata ajira.



