Monday , 27th Feb , 2023

Kampuni  ya VIVO ENERGY  inayojihusisaha na uuzaji wa nishati ya mafuta kupitia vituo vyake vya ENGEN hapa nchini , imeazimia kuboresha mazingira kwa  kupanda miti takribani  1,000 kwenye shule za Dar es salaama na Pwani

Lengo kubwa ni pamoja na kusaidia kutunza mzingira na kuelimisha wanafunzi juu ya umuhimu wa mazingira.

Akizungumza wakati wa utekelezaji wa kampeni iliyopewa jina la panda mti ishi kijani, ambayo ilianza  katika shule ya sekondari ya shushila ladwa iliyopo bagamoyo mkoani pwani, ambapo jumla ya miti 100 ilipandwa, Mkuu wa mkitengo cha masoko na mawasiliano kutoka VIVO ENERGY Bi. Grace Kijo amesema kwamba  Mpango ni kuendeleza kampeni hiyo kwenye shule mbalimbaali nchini na kwamba miti zaidi ya 1,000 inatarajiwa kupanda

Nae Saidi Ling’wala-  ambaye ni Mkuu wa kitengo cha mazingira kutoka  VIVO ENERGY , pamoja na Marco Masaka Meneja vilainishi VIVO ENERGY, w amesema kwamba wakati huu ambapo mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri kilimo kutokana na ukosefu wa mvua, kampuni hiyo imedhamiria kuendeleza ikiwezekana kufikia nchi nzima, lengo likiwa ni kupunguza tatizo hilo

Nao wakizingumza kutoka shuleni hapo ambapo miti hiyo 100 imepandwa   Meshack Jacob ambaye ni  Mkuu wa sekondari   Shushila Ladwa pamoja na Zephania Mtebe Mwanafunzi Shushila Ladwa    wamesema kwamba watakua msitari wa mbele katika kuitunza miti hiyo ili iweze kudumu muda mrefu,na kwamba kupitia miti hiyo mazingira ya shule yataendelea kuwa bora