
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia Nape Nauye katika ziara yeke maalum kwa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampunia ya IPP East Africa Television,East Africa Radio,Itv,Radio One,capital Radio na magazati ya nipashe na the Guardian ambapo katika ziara hiyo amekiri na kusifu uwekezaji mkubwa uliofanyika akisema kuwa IPP iko na washindi wabobevu hivyo kuwaomba kuwa kuendelea kutoa maoni yao katika kamati iliyoundwa ili kupata sheria ya habari itakayokidhi matakwa ya wadau wote.
Nape amevitaka vyombo vya habari kutumia fursa ambazo serikali imezitoa akisifu utashi wa kisiasa ambao Rais Dkt samia Suluhu Hassan amejipambanua, huku akiwataka viongozi wa serikali wenye tabia ya kunyanyasa na kuwatenga waandishi wa habari kwenye maeneo yao kuacha tabia hiyo kwa kuwa hawatafakari ndoto ya Rais.
Kuhusu zoezi la uhakiki wa laini za simu umefanikiwa na kwamba mkakati wa sasa ni kuendelea kuweka mazingira ya chini zaidi kwa watanzania kupata vifurushi nafuu zaidi kwa kuwa linalotumika sasa ni tafiti uliofanyika mwaka 2018.
Waziri Nape amehitimisha ziara yake katika vyombo habari vya IPP akiridhishwa na utendaji ,mifumo,na nia ya dhati ya kuwahabarisha umma kupitia uwekezaji iliofanywa.