Saturday , 4th Mar , 2023

Takriban watu 17 wamepoteza maisha kutokana na moto mkubwa uliotokea katika ghala la mafuta linaloendeshwa na serikali katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta. Watu 60 walijeruhiwa huku watu wengi wakiungau vibaya.

Taarifa zinasema moto huo ulianza mwendo wa saa nane mchana siku ya Ijumaa kutoka kwenye bomba la mafuta katika kituo cha kuhifadhi mafuta cha Plumpang, kinachoendeshwa na kampuni ya mafuta na gesi ya serikali ya Pertamina katika mji mkuu wa Jakarta.

Moto huo ulisambaa haraka  hadi kwenye nyumba za karibu karibu na eneo lenye watu wengi katika kitongoji cha Tanah Merah, na kuwafanya wakazi kuwa na hofu.

 Mamia ya watu wanaoishi katika maeneo ya makazi karibu na moto huo walilazimika kuhamishwa.

Maafisa wa Indonesia wanatoa wito wa ukaguzi wa vituo vyote vya mafuta na miundombin nchini humo.