Tuesday , 28th Mar , 2023

Jeshi la  Polisi Mkoa wa Ruvuma limekabidhi jumla ya lita 630 kwa uongozi wa kampuni ya  CHINA RAILWAY GROUP  inayojihusisha na mradi wa ujenzi wa barabara  ya kiwango cha lami ya Amanimakolo - Ruanda ambayo  yalikamatwa yakiwa yanasafirishwa.

Baada ya kuibiwa yalisafirishwa kutoka katika mradi huo kwa nia  ya kwenda kuyauzwa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma  ACP- Marco  G. Chilya   amesema kuwa  mafuta  hayo yalikamatwa, ambapo watuhumiwa walipelekwa mahakamani ambapo baada ya kesi hiyo kumalizika kwa mtuhumiwa kupata adhabu ya kifungo, mahakama  iliamuru mafuta hayo yarudishwe kwenye uongozi wa unaosimamia mradi ili waweze kuyatumia katika ujenzi huo unaoendelea katika kijiji hicho cha Amanimakolo.

 

Pamoja na hilo Kamanda Chilya ameendelea kutoa onyo kali kwa wale wote  wanaoendelea kujihusisha na uhalifu wa wa kuhujumu mradi huo waache mara moja kwani Jeshi la Polisi Mkoa Ruvuma litahakikisha linawasaka, kuwakamata pamoja na kuwafikisha mahakamani  kama ilivyokuwa kwa wahalifu wengine. 

 

Jeshi hilo limewahakikishia Raia hao wa kigeni kuwa linaendelea kufanya Misako, doria na Operesheni mbalimbali kuhakikisha maeneo yote ya Mkoa yanakuwa salama ikiwa pamoja na eneo lao la Ujenzi wa barabara.