
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei hizo mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia leo Jumatano Mei 3, 2023
Hata hivyo katika mikoa ya kaskazini ikijumuisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara bei za mafuta ya petrol na dizeli zitasalia kama ilivyokuwa Aprili Sh2,756 na Sh2,900
Taarifa ya (Ewura) imeeleza kuwa utofauti wa bei katika mikoa inasababishwa na umbali wa usafirishaji wa mafuta kutoka bandarini na bandari ambayo mkoa husika unachukua mafuta hayo
Kwa upande wa mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Mtwara ambayo inahusisha mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) bei ya mafuta ya petroli na dizeli ya rejareja itabaki kama ilivyokuwa Aprili kwasababu hakuna shehena mpya ya mafuta iliyopokelewa.
Kwa mwezi huu bei ya mafuta itakuwa juu zaidi katika Wilaya ya Kyerwa ambapo petroli inauzwa Sh3,109 na dizeli inauzwa Sh3,109 hii inasababishwa na umbali uliopo kutoka bandarini.