Thursday , 4th May , 2023

Mabasi ya Mikoani yameruhusiwa kuanza  safari zake saa tisa usiku ambapo Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeagiza Wamiliki wa Mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wafike katika Ofisi zao kuomba leseni

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy amesema ni lazima Madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao

"Tunafanya kazi kwa kushirikiana, suala la kubadilisha ratiba za Mabasi awali muda ulikuwa ni yote lazima yaanze safari saa 12 asubuhi si zaidi ya hapo, lakini baadaye tuliruhusu ratiba zianze saa 11 asubuhi”