Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Utalii wa Bahari kunufaisha wavuvi

Friday , 23rd Jun , 2023

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema  Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira mazuri kupitia fursa za Utalii wa Bahari ili wavuvi hasa  wadogo waweze kunufaika kwa kuuza samaki na mazao yake.

Waziri Ulega alisema hayo wakati wa tukio la mashindano ya Ngalawa (Ngalawa race) lililofanyika kwenye ufukwe wa Kendwa uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja Juni 22, 2023.

Alisema kuwa kupitia mashindano hayo shughuli za uvuvi zitatangazika duniani na kuvuta watalii wengi na  hivyo wavuvi  watapata fursa nzuri ya  kufanya biashara ya samaki.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yanachagiza ujio wa watalii nchini na hivyo kupelekea utalii wa bahari  kushamiri kitendo ambacho kinaongeza fursa ya biashara kwa  wavuvi.

"Tunataka huu utalii wa bahari  uwanufaishe moja kwa moja wavuvi wadogo waweze kupata kipato chao kutokana na mauzo ya samaki na mazao yake kwa watalii hao," alisema

Aidha, Mhe. Ulega aliwashauri wavuvi  kutumia vyema mwambao wa Bahari kwa kuanza kufanya shughuli mbadala za kujiongezea kipato ikiwemo ufugaji wa Kaa, Kambakochi na Majongoo Bahari.

Alisisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwainua wavuvi na ndio maana inafanya kila jitihada za kuboresha shughuli zao ili ziwe na mchango mkubwa na thamani yake ionekane kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90