Nyama
Pamoja na kujadiliana mambo mengine, suala la biashara ya nyama kutoka Tanzania kwenda kuuzwa nchini Misri lilijadiliwa kwa kina huku Mhe. El Kosayer akiahidi kulifanyia kazi kwa haraka ili biashara hiyo iweze kuleta matunda kwa pande zote mbili.
Mapema wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Kosayer alimueleza Waziri Ulega kuwa lengo la kukutana kwao ni kuona namna wanavyoweza kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.