Wednesday , 22nd Nov , 2023

Ukifikiria kiundani juu ya ule msemo wa mwenye bahati habahatishi basi utaelewa dhana nzima ya mwamba wa kuitwa Sam Altman

 

Ila wapo wahenga waliokuja kushusha hadhi ya msemo huo kwa kusema juhudi na fursa vikikutana kwa pamoja ndiyo hutengeneza kitu kinaitwa bahati

Wakati hatujui tushike kipi, mara tunapata taarifa mpya ya kwamba yule mtoto aliyechapwa akakimbia kwao Baba amesema arudishwe nyumbani.

Tungo za kiswahili zisiwe nyingi, Mtoto mwenye ni Sam Altman ambaye awali alihudumu kama mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya OPEN.AI, nasema awali kwa sababu alikwisha fukuzwa kwenye nafasi hiyo na yeye akachagua kuhamia upande wa pili

Unaweza kuhisi tunachanganya mambo ila unaweza kusoma mwanzo mwa haya tunayozungumza hapa.
Web: https://eatv.tv/news/life-style/hajui-kuhusu-msoto-wa-kupata-kazi

Upande wa pili ambao Sam alichagua ni kampuni ya Microsoft lakini siku chache baada ya kupewa nafasi kwenye kampuni ya Microsoft, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Satya Nadella, alitoa mapendekezo yake ya kwamba ingefaa zaidi Sam akirejea kwenye nafasi ya ukurugenzi ndani ya kampuni ya Open A.I kwani wote wanajenga nyumba moja.

Kwenye hiyo link, hapo juu nimeeleza kwa nini aliweza kuwa na nafasi ya ndani ya kampuni ya Open A.I ikiwa yeye ni mkurugenzi wa Microsoft,

Baada ya kiti cha ukurugenzi ndani ya kampuni hiyo kupata mkurugenzi wa muda ambaye ni Mira Murati, bodi ilikaa tena nakuona iko haja ya kumrejesha Sam kwenye nafasi yake 

Kwani moja zaidi ya wafanyazi 500 ndani ya kampuni hiyo walitishia kugoma hata kuacha kazi ikiwa hatorejeshwa kwa aliyewahi kuwa Boss wao.

Mbili ni baadhi ya wanahisa kama vile Microsoft kukaa kwenye bodi na kuona ipo haja ya Sam, kurejeshwa kwenye nafasi yake.

Hivyo bodi mpya ya wakurugenzi hivi sasa itaundwa na Taylor na wajumbe wengine kama Larry summer, Adam D'angelo na wengineo.

Kwa ukumbusho tu baada ya Sam kurudishwa kama mkurugenzi ndani ya kampuni hiyo, mwanzilishi mwenza ambaye wote walienda upande wa pili (Grey Brockman) naye amerejea ndani ya kampuni hiyo

Picha: redian.news|