Tuesday , 28th Nov , 2023

Uaminifu ni kitu muhimu kwenye mahusiano ikiwa ni kwako mwenyewe au kwa mtu mwingine, muziki umekuwa sehemu kubwa kwenye kumkumbusha mwanadamu kuhusu mambo/vitu mbalimbali.

Kutoka zamani na hata sasa, kuna burudani nyingi za muziki ambazo zimegusia suala la uaminifu kwenye mahusiano kama vile; Shawn Mendes -Honest, Kendrick Lamar - Loyalty, Chris Brown & Tyga & Lil Wayne - Loyal.

Lakini hapa nakurudisha nyuma miaka 4 iliyopita kwenye burudani ya Be Honest – Jorja Smith ft Burna Boy

Jorja anajaribu kueleza hisia za kumuamini mtu kwenye mahusiano lakini unagundua mtu huyo si muaminifu,

Lakini mwishoni Jorja anasema ipo nafasi ya kurekebisha hilo kwani wanadamu wote tunafanya makosa, hivyo tunaweza kurekebisha kwenye suala la uaminifu kwa wewe mwenyewe kuwa muaminifu.

Picha: abouther.com