Friday , 1st Dec , 2023

Kwenye mahojiano yake na Dua Lipa kwenye Podcast ya ''At your service'' mtendaji mkuu wa kampuni ya Apple inc, Tim Cook alifunguka aina ya watu ambao hupenda kuwaajiri kwenye kampuni hiyo.

Ukitoa kigezo cha shahada Tim cook alifunguka kwa kusema kwa upande wa kampuni ya Apple Inc tunaajiri watu kutokea sehemu tofauti,

Wale wenye shahada, wasio na shahada, wale wanaofahamu kuhusu coding hata wale wasiyo fahamu.

Lakini kuna vigezo vitatu ambavyo yeye kama mtendaji mkuu anasimamia kwenye kuajiri watu kwenye kampuni hiyo

1. Ni uwezo wa mtu kushirikiana na watu wengine (collaboration)

2. Mdadisi: Tim anasema anapenda sana mtu ambaye anauliza maswali wanapokuwa pamoja kama timu

3. Mbunifu: Tim anasema APPLE wanatazama watu ambao wanauwezo wakutazamia nje ya yale yaliyokuwako (jicho la tatu)

Yote haya kwa pamoja yanatengeneza, timu ya watu makini kwa mujibu wa Tim, kwa upande wako unahisi mtazamo wa Tim uko sahihi kiasi gani?