Saturday , 27th Apr , 2024

Mwanamke mwenye umri wa miaka 58 nchini Kenya katika shamba la Sifa Kitengela amekamatwa na polisi baada ya kuishi na mwili (maiti) ya mume wake ndani kwa muda mrafu mpaka mwili huo ukaharibika akiamini kuwa iko siku atafufuliwa.

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini humo, mwanamke huyo amekamatwa baaada ya majirani zake kuripoti juu ya uwepo wa harufu mbaya ambayo si ya kawaida iliyokuwa ikitoka kwenye nyumba walioyokuwa wanaishi wanadoa hao.

Inaelezwa kuwa baada ya mwanamke huyo kuwazuia Polisi kuingia ndani, maofisa hao wa Polisi walilazimisha kuingia kwa nguvu kwenye nyumba hiyo na kukuta maiti ya mumewe ikiwa imelala karibu na kitanda chake sebuleni.

Mwanamke huyo anadaiwa kukaa kwenye milango muda mwingi, na kutokuwasiliana na jirani anatajwa kuwa ni miongoni mwa wafuasi wa madhehebu ya kidini ambayo yalizuia ulaji wa vyakula, isipokuwa ndizi na maji na pia imani yake haikumruhusu kupata watoto.

Kwa sasa mwanamke huyo amepelekwa katika hospitali ya Mathare kwa matibabu na kufanyiwa uchunguzi, huku mwili wa mumewe ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City akisubiri kuzikwa nyumbani kwake Nyeri.