Monday , 6th May , 2024

Ajali hiyo imetokea Mei 6 2024 majira ya saa 7:00 mchana katika eneo la Mbembela mkakabala ya kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Indente.

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watu watatu wamenusurika kifo baada gari namba T 422 AKF  yenye  tela T303 APW Scania lilokuwa nimebeba shehena ya mchele likitokea Jijini Dar-es-salaam kuelekea nchini ya Zambia baada ya kumgonga mwendesha bodaboda na badaye kuacha njia na kupinduka katika eneo Mbembela kata ya Nzovwe jijini Mbeya barabara kuu ya Mbeya -Tunduma.

Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu watatu wamejeuriwa na wote wapo Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wakiendelea kupatiwa matibabu.