Thursday , 12th Mar , 2015

Uongozi wa Klabu ya Yanga umekanusha juu ya suala la kuwachukulia hatua wachezaji baada ya kufungwa na timu ya Simba bao 1-0 katika muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara iliyochezwa Machi nane Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema, kwa sasa hawana mpango wa kumlaumu mchezaji yoyote au kocha ambaye wamekaa nao kikao kwa ajili ya kuwapa lawama za kuihujumu timu katika mchezo huo.

Murro amesema, kama kunamchezaji ameonekana kuchangia timu kufanya vibaya, zipo sheria lakini hivi sasa wanaangalia mbele kwa ajili ya michuano inayofuata ili waweze kurekebisha makosa yaliyopo katika timu ili timu iweze kufanya vizuri zaidi.

Murro amesema, kwa Upnde wa Mchezaji Danny Mrwanda, alishikwa na Maralia baada ya mechi dhidi ya Simba na hivi sasa anaendelea na matibabu na hatoweza kucheza mechi ya Jumapili dhidi ya Platinums kwasababu anakadi nyrkundu aliyoipata Gaborone katika Mechi na Timu ya Botswana.

Murro amesema, hivi sasa hali ya Nahodha Nadir Haroub Canavaro inaendelea vizuri na anapata matibabu ya karibu kwa ajili ya kuendelea kutibu sehemu aliyoumia ambapo ni karibu na jicho baada ya kuumia akatika mechi dhidi ya Simba.