Saturday , 10th May , 2025

Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) siku ya Ijumaa limetangaza kuahirisha mechi ya Ligi Kuu nchini humo "Mashemeji Derby" baina ya Gor Mahia na AFC Leopards ambayo iliratibiwa kuchezwa Jumapili, Mei 11, 2025.

Kupitia taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo ilieleza kuwa uamuzi huo umefanyika kutokana na kukosekana kwa uwanja unaokidhi mahitaji ya usalama. Pia iliongeza kuwa uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambao ulikuwa umependekezwa kutumika kwa ajili ya mchezo huo ulifungwa na Shirikisho la mpira Afrika (CAF) kwa kuwa unakarabatiwa kwa ajili ya maandalizi ya dimba la CHAN 2025.

Kutokana na hayo, FKF na wawakilishi wa timu zote (Gor mahia na AFC Leopards) walifanya mkutano siku ya Ijumaa. Timu hizo zilijulishwa uamuzi huo na sababu zilizopelekea mechi hiyo kuahirishwa.

FKF ilisema kuwa itawasilisha tarehe mpya kwa wakati ufaao.