Tuesday , 27th May , 2025

Mwanamuziki wa Kenya Bien Sol ameweka historia ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Africa Mashariki kuonekana na kusikika kipindi kikubwa cha radio Marekani The Breakfast Club.

Picha ya Bien Sol

Akizungumzia safari yake ya muziki Bien anasema "Nilianza kupenda muziki nikiwa na miaka mitano au sita, nilikuwa naangalia muziki wa Bob Marley nikahisi kupenda kufanya hii kitu".

"Sasa hivi nina miaka 37 nimeanza kuimba nikiwa na miaka 6, na nilijiunga na kwaya ya kanisani na kanisa ndio program bora zaidi ya ukuzaji wa wasanii ulimwenguni sababu linatoa wanamuziki wa Wakubwa hasa kwa muziki wa watu weusi".

Mengine ambayo amefunguka ni kuhusu soko la muziki Africa na Marekani,tuzo za Grammy, kumuoa Meneja wake, kundi la Sauti Sol kurudi na nguvu ya Marekani kwenye muziki.