
"Jina la sharobaro ya BobJ unior, Oh mama ya Sharo Milionea Mdebwedo ya Joti ni za kwangu na uzuri na ubaya wa vitu vingi ambavyo nimevifanya vingi sikuwahi kufikiria katika upande wa kulipwa, Kwasababu hata sisi wenyewe huko nyuma tumeibiwa sana mirabaha za kazi zetu tulikuwa hatujui hata kama tunatakiwa kulipwa kwahiyo dunia inavyozidi kwenda ndio tunapata elimu ya vitu kama hivyo'' amesema Dully Sykes
"Sijawahi kufollow mtu mimi (Instagram) ila huwa nwaangalia (Profile zao) halafu naachana nao kuna wale watu ambao wanatukana kwenye komenti huwa naenda naangalia maisha yao halafu nacheka, Huwa napenda sana kuangalia maisha ya mtu ambaye ananitukana pengine niangalie kama amenizidi hata miaka ila sio maendeleo lakini nikija kuangalia nakuta nimewazidi Miaka, maendeleo,dhambi mpaka thwawabu nimewazidi" amesema Dully Sykes