
Jadon Sancho
Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na United 2021 akitokea Borussia Dortmundkwa ada ya pauni milioni 73 huku akijiunga na Chelsea kwa mkopo msimu uliopita baada ya kutokuwa na uhusiano mzuri dhidi ya Erik ten Hag aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United.
Chelsea wanalazimika kulipa faini hiyo baada ya kukubali kumnunua Sancho kwa ada ya takribani pauni milioni 25 ikiwa wangemaliza kwenye nafasi 6 za juu za EPL lakini baadae wakabadili mpango huo.