
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa mchezaji muhimu kwa klabu tangu ajiunge nayo kutoka Lille mwaka 2020, na amefanikiwa kucheza mechi 210 katika mashindano yote mpaka sasa huku akifunga mabao 17 kwenye ligi ya EPL.
Gabriel ndiye aliyefunga mabao mengi zaidi ya vichwa (12) na kutengeneza clean sheets (57) kati ya mabeki wote wa Premier League tangu acheze mechi yake ya kwanza. Ikumbukwe tangu 2022, Gabriel ameunda ushirikiano mzuri na William Saliba kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal, huku wote wawili wakionekana kuwa tishio zaidi.