Monday , 16th Jun , 2025

Naibu Inspekta Generali (DIG) wa Huduma ya Polisi ya Kenya, Eliud Kipkoech Lagat, ametangaza rasmi kujiondoa katika nafasi yake wakati uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kifo chenye utata cha blogger Albert Ojwang

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Lagat amesema kwamba uamuzi wake umetokana na uzito wa ofisi yake na maslahi ya umma yanayohusiana na kesi hiyo.

“Leo nimeamua kujiondoa kutoka ofisi ya Naibu Inspekta Generali - Huduma ya Polisi ya Kenya, hadi kukamilika kwa uchunguzi,”

“Majukumu ya ofisi hiyo yatatekelezwa kuanzia sasa na naibu wangu hadi uchunguzi utakapokamilika. Ninaahidi kutoa msaada wowote ambao unaweza kuhitajika kutoka kwangu wakati wa uchunguzi wa tukio hili la kusikitisha,” amesema Lagat