
Picha ya msanii Zee Cute
Taarifa hiyo inaeleza
"Kwa heshima kubwa ya familia na meneja wa Zee Cute inawataarifu vyombo vya habari,mashabiki na wadau wote wa tasnia ya muziki kwamba msanii wetu kwa sasa yupo chini ya uangalizi na matibabu maalum kutokana na changamoto za kiafya hususani zinazohusisha afya ya akili ambazo amekuwa akikabiliana nazo katika kipindi hiki".
Siku kadhaa zilizopita Zee Cute mwenyewe aliandika ujumbe wa kuhitaji msaada wa afya ya akili sababu anapitia changamoto hiyo.