Monday , 23rd Jun , 2025

Shai Gilgeous-Alexander mchezaji nyota wa timu ya The Oklahoma City Thunder ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa fainali ya ligi ya mpira wa kikapu Marekani NBA (NBA Final MVP) 2025. Pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 11 kushinda tuzo ya MVP wa Ligi (regular-season) na MVP wa fainali

Shai Gilgeous-Alexander

Ameshinda tuzo hii baada ya kuisaidia timu yake ya The Oklahoma City Thunder kushinda ubingwa wa NBA msimu huu 2024-25 baada ya kushinda mchezo wa saba wa fainali leo alfajiri kwa kuifunga Indiana Paceres kwa alama 103-91, na kushinda fainali kwa ushindi wa michezo 4-3.

Kwenye mchezo huu wa saba Shai Gilgeous-Alexander amecheza dakika 40, kafunga alama 29, katoa pasi za kufunga (assist) 12 na mipira iliyorudi yani reboundi 5.