Monday , 28th Jul , 2025

Kuna watu waliowahi kukumbwa na hatari kuu kiasi cha kuonekana kama mwisho wa safari yao ya maisha, lakini kwa namna ya ajabu waliendelea kuvuta pumzi hawa ni baadhi kati ya hao

 

1. Tsutomu Yamaguchi
Yamaguchi ni jina lililoandikwa kwa wino wa kudumu kwenye historia ya dunia. Alikuwa Mjapani wa kawaida lakini alipata mshtuko wa maisha aliponusurika bomu la atomiki la Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945 na siku tatu baadaye akanusurika tena kwenye bomu la pili huko Nagasaki alitambuliwa rasmi na serikali ya Japan kuwa manusura pekee wa mashambulizi yote mawili.

2. R. Norris Williams
Williams hakuwa tu nyota wa tennis wa Marekani, bali pia alikuwa abiria wa Titanic. Wakati meli hiyo maarufu ilizama mwaka 1912, alinusurika maji ya baridi kali ya Atlantiki. Miguu yake ilikaribia kukatwa kutokana na baridi kali, lakini alikataa, akapona, na baadaye akashinda mashindano makubwa ya tennis akigeuza janga kuwa ushindi.

3. Jacob Miller
Katika mapigano makali ya Chickamauga huko Georgia mwaka 1863, Jacob Miller alipigwa risasi katikati ya paji la uso akiwa askari wa jeshi la Union. Alinusurika na aliishi kwa miaka mingi na risasi kichwani, akijulikana kama “askari aliyebeba risasi kichwani hadi uzee”.

4. Ndumiso Mona
Mwanaume huyu kutoka Afrika Kusini ameacha wengi midomo wazi baada ya kuripotiwa kupambana uso kwa uso na chui na kumuua kwa mikono yake. Tukio hilo limevuma mtandaoni na kuwa ushahidi wa ushujaa wa kipekee na jitihada za kupambana na mauti kwa mikono mitupu.

Kwa kifupi: Hawa ni mashujaa waliogusa ukingo wa kifo lakini wakarejea tena.