Trump anatarajiwa siku ya Jumanne kukutana na Waziri Mkuu wa wa Japan Sanae Takaichi katika mkutano wenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na Japan.
Ziara ya Trump barani Asia imekuwa pia fursa ya kusaini mikataba kadhaa ya kibiashara kabla ya kuhudhuria pia siku ya Jumatano mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya nchi za Asia-Pasifiki, APEC katika mji wa Gyeonju nchini Korea Kusini.
Trump atakamilisha ziara yake barani Asia kwa kufanya mkutano wa kilele na Rais wa China na Xi Jinping siku ya Alhamisi huko Korea Kusini ambapo viongozi hao wanalenga kutafuta suluhu ya miezi kadhaa ya vita vya kibiashara.
