Monday , 17th Nov , 2025

Jumuiya ya burudani nchini Tanzania imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha ghafla cha mchekeshaji na mshereheshaji maarufu, Emmanuel Mathias, anayefahamika zaidi kwa jina la MC Pilipili.

 

MC Pilipili amefariki dunia Novemba 16, 2025, jijini Dodoma, ambapo alikuwa amewasili kwa ajili ya shughuli za kazi.

Marehemu alikumbana na mauti hayo kabla ya kuanza shughuli zake za ushereheshaji alizokuwa amepanga kuzifanya siku ya jana jijini Dodoma.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi.

"MC Pilipili amefikishwa katika hospitali yetu akiwa tayari amefariki dunia," Ibenzi ameeleza.

Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya burudani, ambapo alitambulika kwa uwezo wake wa kipekee wa kuchekesha na kuongoza matukio mbalimbali.