Monday , 23rd Feb , 2026

UEFA imemsimamisha Kiungo wa Benfica Gianluca Prestianni kwa mchezo mmoja dhidi ya Real Madrid huku uchunguzi wa kesi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Vinicius Jr katika mchezo wa awamu ya kwanza wa "Playoff" ya UEFA CL 

Vinicius Jr na Jose Mourinho

Taarifa rasmi ya UEFA bado wanaendela kuchunguza madai ya ubaguzi wa Rangi yanayomkabili Gianluca Prestianni. Ikiwa madai yatathibitishwa, Prestianni anaweza kukabiliana na adhabu ya kufungiwa Michezo 10 na faini.

Mechi ya kwanza ya wiki iliyopita ilisitishwa kwa dakika 10 baada ya Vinicius kumjulisha mwamuzi wa uwanjani Letexier kuhusu tukio hilo la kipindi cha pili, kabla ya yeye na wenzake kuondoka uwanjani kwa muda.

Meneja wa Benfica Jose Mourinho, ambaye amesimamishwa kucheza mechi ya marudiano baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu baadaye katika mechi hiyo, alikosolewa kwa matamshi yake baada ya kusema anaamini Vinicius alikuwa ameshangilia bila heshima

Real Madrid na Benfica watakutana kwa ajili ya mchezo wa marudiano katika mji mkuu wa Uhispania siku ya Jumatano